Testimonials!

Alistidia Kamugisha
★★★★★

Alistidia Kamugisha

Community Transformation Alliance (CTA)

“Kwa maoni yangu kama mdau wa elimu kubadilishwa kwa ratiba ya mitihani ni uamuzi wenye tija kwani majanga hayatabiriki na ni bora sana wizara imechukua tahadhari na kuamua hivyo ushauri wangu, jamii ielimishwe juu ya maamuzi haya na pia wazazi wawasaidie watoto ili waweze kujiandaa katika hali hii ya udharura na kufanya vizuri mitihani yao.”

Mahmudi Ngamange
★★★★★

Mahmudi Ngamange

Ofisa Mthibiti ubora Elimu

“Ujumbe wangu kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani, someni kwa bidii wakati mnajiandaa na mitihani yenu na pia endapo mvua zitaanza kunyesha epukeni kutembea sehemu za hatari wakati wa mvua.”

Emanuel Shilembi
★★★★★

Emanuel Shilembi

Mzazi

“Wizara iangalie na kusimamia kwa umakini hili swala la mabadiliko ya ratiba za mitihani, sababu baadhi ya shule wanaweza wakachulia hii kama nafasi ya kusaidia kwa njia zisizo sahihi na kuwapitisha hata watoto wasio na uwezo kimasomo. Kumbuka mitaala ina vigezo na masharti ya kuwa mwanafunzi ili ahitimu anapashwa kusoma siku kadhaa shuleni na kufanya majaribio na mitihani kadhaa kabla ya kufanya mitihani husika ya Necta”

Bi, Nashivai Mollel
★★★★★

Bi, Nashivai Mollel

CEO, Transforming Life (TL)

Ningeshauri pia shule ziwe na mipango mbadala ya kuhakikisha ujifunzaji unaendelea iwapo hali ya hewa itakuwa mbaya, hasa kwa maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua kubwa au changamoto za usafiri. Mawasiliano ya wakati na ya wazi kutoka kwa mamlaka za elimu, shule, walimu na wazazi ni muhimu sana ili kupunguza hofu na mkanganyiko

Evena Massae
★★★★★

Evena Massae

CEO, COSUPED NG'OS

“Nashauri viongozi wa  elimu Tanzania na watu wa usalama katika ngazi zote, pamoja na  walimu, wanafunzi, wazazi  na wadau mbalimbali wa elimu washirikiane na kila mmoja atimize wajibu wake katika kipindi hiki tunapoelekea kipindi cha mvua za elnino. Kwa umoja huo watahakikisha mitihani inafanyika vizuri kukiwa na utulivu, usalama na amani. Mungu Iibariki Taifa la Tanzania.”