Shule Zote Kufungwa Tarehe 13 Novemba 2026

Kamishna wa Elimu nchini, Dkt. Lyabwene M. Mtahabwa  ameelekeza kwamba, Shule zote zifungwe tarehe 13 Novemba 2026 kwa muhula unaoishia Desemba, 2026 badala ya tarehe 04/12/2026 kama ilivyokuwa imeelekezwa awali katika nyaraka za Elimu zilizotolewa hapo awali.

Maelekezo hayo ya kamishna yametolewa kupitia Waraka wa Elimu na. 3 wa Mwaka 2026 kuhusu mabadiliko ya tarehe ya kufunga shule za awali, msingi na sekondari Tanzania bara. Waraka huo uliotolewa mwishoni mwa wiki hii, umeelekeza kwamba utaanza kutumika rasmi tarehe 1 Oktoba, 2026.

Aidha waraka huo unaeleza kuwa uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu uwezekano wa mvua kubwa za El Nino na athari zake na kubainisha kwamba hatua hii inalenga kulinda usalama na ustawi wa wanafunzi, walimu na watumishi wengine katika shule.

 

About Admin 9 Articles
EC Magazine, whose full name is Elimu (Education) Communication Magazine, is an online educational magazine dedicated to reporting and publishing education news, insights, research, impacts, and developments across Tanzania, Kenya, and Uganda.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*