RC Kheri James Apongeza Maboresho ya Miundombinu MUCE

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, ametoa pongezi kwa kasi na ubora wa utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi na maboresho ya miundombinu ya elimu wenye thamani ya Shilingi Bilioni 30.4 katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), mradi unaotarajiwa kuongeza fursa za udahili na kuboresha mazingira ya taaluma kwa wanafunzi na wakufunzi, kupitia miundombinu ya kisasa inayokidhi viwango vya kimataifa.

Kwa Mujibu wa chombo cha Habari cha mtandaoni kijulikanacho kwa jina la FocusTV Tanzania, kama walivyochapisha hivi karibuni katika Ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa Mkuu wa mkoa akiwa katika ziara yake maalum chuoni hapo iliyolenga kujionea kwa macho na kukagua hatua zilizofikiwa, RC Kheri James amejionea ujenzi wa majengo ya kisasa yanayohusisha madarasa ya kufundishia, hosteli za wanafunzi, maabara za sayansi, maktaba ya kisasa pamoja na majengo ya idara mbalimbali.

RC Kheri James ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa MUCE kwa usimamizi thabiti na uwazi katika matumizi ya fedha hizo za serikali, huku pia akiwapongeza wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kwa kuonyesha viwango vya juu vya umahiri na kasi inayoridhisha.

  Naamini picha zote unazo. Jana nilituma. kama kuna mahala zitakuchanganya nipigie kabla hujaweka.

About Admin 9 Articles
EC Magazine, whose full name is Elimu (Education) Communication Magazine, is an online educational magazine dedicated to reporting and publishing education news, insights, research, impacts, and developments across Tanzania, Kenya, and Uganda.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*