Njombe, Uwezo Kushirikiana Kutatua Changamoto ya KKK kwa Wanafunzi

Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na Shirika la Uwezo Tanzania lenye makao makuu jijini Dar es Salaam, wamefanya mafunzo ya walimu na wawezeshaji kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa Mradi wa Kijiji Changu (My Village Project) Awamu ya IV, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), pamoja na stadi za maisha na maadili kwa watoto wa miaka 5 hadi 17.

Mafunzo hayo yaliyofanyika wilayani Makete yaliwalenga walimu ambao watatumia mbinu ya shirika la Uwezo Tanzania ya Jifunze ili kusaidia watoto kwa kuzingatia kiwango chao halisi cha ujifunzaji na kufuatilia maendeleo yao hatua kwa hatua.

Aidha, taarifa iliyotolewa na shirika la Uwezo Tanzania kwa waandishi wa Habari wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo inasema, hatua hii inakuja wakati takwimu za Mkoa wa Njombe za mwaka 2026 zinaonesha kuwa Mkoani Njombe, miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 10–14, takribani watoto 6 kati ya 10 wanafikia kiwango cha chini cha umahiri katika kusoma, na watoto 7 kati ya 10 katika kuhesabu. Hii ina maana kuwa bado watoto 4 kati ya 10 hawajafikia kiwango cha chini cha umahiri katika kusoma, na 3 kati ya 10 katika kuhesabu.

“Changamoto yetu si kuhakikisha watoto wako shuleni pekee, bali kuhakikisha watoto walioko shuleni wanajifunza. Tunahitaji kujua mtoto yupo katika kiwango gani cha ujifunzaji,wapi anakwama na kutumia matokeo hayo ya tathmini tutatumia mbinu ya Jifunze kuongeza umahiri wake katika KKK.” Baraka Mgohamwende – Mkurugenzi Mkuu, Uwezo Tanzania.

About Admin 9 Articles
EC Magazine, whose full name is Elimu (Education) Communication Magazine, is an online educational magazine dedicated to reporting and publishing education news, insights, research, impacts, and developments across Tanzania, Kenya, and Uganda.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*